Jumamosi, 29 Aprili 2017
SSRA YASHIRIKI MAONYESHO YA MAADHIMISHO YA SIKU YA USALAMA NA AFYA MAHALA PA KAZI MJINI MOSHI MKOANI KILIMANJARO
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi, na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) Bi Amina Ally aliotembelea banda la SSRA wakati wa Maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi (OSHA) yanayoendelea mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama akiatoa maelekezo wakati alipotembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwenye Maonyesho ya Maadhimisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi (OSHA) yanayoendelea mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira, Kazi na Watu wenye Ulemavu, Mh. Jenista Mhagama, akimkabidhi cheti cha Ushiriki Kaimu Meneja wa Rasilimali watu na Utawala wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA). Bi. Amina Ally wakati wa kilele cha maonesho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayoendelea Mjini Moshi, mkoani, Kilimanjaro.
Afisa Matekelezo wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), akigawa vipeperushi kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA wakati wa Maonesho ya OSHA yanayondelea Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Afisa Uhusiano na Uhamasishaji wa Mamlaka ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Bw. Ally Masaninga akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la SSRA, wakati wa Maonesho ya OSHA yanayondelea Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Maafisa wa SSRA, wakitoa ufafanuzi juu ya Masuala yanayohusu Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa wadau waliotembelea banda la mamlaka hiyo, wakati wa Maonesho ya OSHA, yanayoendelea Mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Wananchi wakisikiliza maelezo kutoka kwa Afisa wa SSRA, wakati wa maonesho ya OSHA, yanayofanyika mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Wadau waliotembelea banda la SSRA, wakijipatia vipeperushi wakati wa maonesho ya Maadhmisho ya Siku ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi yanayofanyika Mkoani Kilimanjaro.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni
(
Atom
)
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni