Timu ya Leicester City imepata
ushindi wa sita wakiwa na kocha mpya Craig Shakespeare baada ya
kuifunga Sunderland iliyokatika mazingira magumu kwa magoli 2-0.
Leicester ilionekana kuwa chini ya
kiwango chao, lakini uamuzi wa kocha Shakespeare kumuingiza Marc
Albrighton na Islam Slimani ulifanya kubadili mchezo huo.
Baada ya dakika saba tu kuingia
dimbani Albrighton alitoa krosi ya wingi ya kushoto iliyotumbukizwa
kichwani kwa kichwa na Mualgeria Slimani.
Albrighton tena alitoka nduki nusu
uwanja na kuachia krosi iliyomkuta Jamie Vardy, aliyeituliza kwanza
na kuachia shuti kali lililojaa wavuni.
Islam Slimani akipiga mpira wa krosi kwa kichwa na kufunga goli
Jamie Vardy akiachia shuti na kufunga goli la pili la Leicester City
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni