.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 27 Aprili 2017

TOTTENHAM YAZIDI KUIPA PRESHA CHELSEA UBINGWA LIGI KUU UINGEREZA

Tottenham imeendelea kuipa presha Chelsea katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kufuatia Christian Eriksen kufunga kwa shuti kali na kuibuka na ushindi dhidi ya Crystal Palace.

Tottenham ilipata wakati mgumu kupasua ngome iliyona nidhabu kubwa ya Palace katika karibi kipindi chote cha mchezo huo wa jana ambao ilionekana kama utaishia kwa sare ya 0-0.

Lakini Eriksen aliachia shuti la umbali wa yadi 30 lililojaa katika kona ya chini ya goli katika dakika za mwisho na kuifanya Tottenham kuwa pointi nne nyuma ya Chelsea.
           Christian Eriksen akiachia shuti ambalo lilizaa goli pekee katika mchezo huo
                        Beki Mamadou Sakho akibebwa kwenye machela baada ya kuumia goti 
Katika mcheo mwingine Arsenal imeendelea kuwania kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza baada ya Robert Huth kujifunga goli katika mchezo ulioishia kwa ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Leicester City.
   Kipa Petr Cech akifanya jitihada za ziada kupangua mpira uliopigwa na Riyad Mahrez

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni