Timu ya Real Madrid imezidi
kujiimarisha kuelekea kutwaa ubingwa wa Ligi ya La Liga, kwa kupata
ushindi wa kishindo wa magoli 6-2 dhidi ya Deportivo la Coruna.
Madrid inayonolewa na Zinedine
Zidane, inapointi sawa na vinara Barcelona lakini wanamchezo mmoja
mkononi na inaweza kutwaa ubingwa iwapo itashinda michezo yote
iliyobakia.
Katika mchezo huo Cristiano Ronaldo
alipumzishwa na Gareth Bale akiwa majeruhi, Madrdid ilipata goli lake
la kwanza kupitia kwa Alvaro Morata katika dakika sekunde ya 54.
James Rodriguez alifunga magoli
mawili likiwemo la kuubetua mpira kiifundi juu ya kipa, pia Lucas
Vazquez, Isco na Casemiro walifunga huku Deportivo wakipata magoli
kupitia kwa Florin Andone na Joselu.
Alvaro Morata akiifungia Real Madrid goli la kwanza
James Rodriguez akiachia shuti na kufunga moja kati ya magoli mawili aliyoyafunga



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni