.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Aprili 2017

UCHAGUZI WA UFARANSA KUFANYIKA LEO CHINI YA ULINZI MKALI

Wapigakura wanapiga kura leo nchini Ufaransa kumchagua rais wao ajaye, huku kukiwa na ulinzi mkali kufuatia shambulizi hatari Jijini Paris siku tatu zilizopita.

Karibu maafisa polisi 50,000 na wanajeshi 7,000 wamesambazwa katika maeneo mbalimbali nchi nzima ya Ufaransa kulinda vituo vya kupigia kura.

Wagombea 11 wanawania kuwa rais ajaye wa taifa hilo, huku wagombea wanaoonekana kutoa ushindani ni wale wenye kufuata siasa za mrengo wa kulia na mrengo wa kushoto.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni