.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 24 Aprili 2017

WAYNE ROONEY AREJEA DIMBANI NA GOLI MAN U IKISHINDA

Wayne Rooney amefunga goli lake la kwanza tangu mwezi Januari wakati Manchester United ikiendelea kufukuzia nafasi ya nne ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa kupata ushindi dhidi Burnley.

Rooney alianza kikosi cha kwanza kwa mara ya pili kwa mwaka huu baada ya kocha Jose Mourinho kufanya mabadiliko nane kutoka kikosi kilichoifunga Anderlecht ligi ya Uropa.

Kapteni huyo wa Uingereza alianza vyema na walifanya shambulizi na kupata goli la kwanza kupitia kwa Anthony Martial na kisha baadaye Rooney alifunga kwa kuupenyeza mpira golini akiwa kwenye eneo gumu kufunga na kuongeza la pili.
                                Anthony Martial akifunga goli la kwanza la Manchester United
                    Wayne Rooney akijipinda na kufunga goli katika eneo gumu kufunga

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni