Ajax imejiweka katika nafasi ya
kuweza kutinga fainali ya kwanza ya Ligi ya Uropa kwa mara ya kwanza
katika miaka 21, kwa kuichakaza Lyon kwa magoli 4-1 katika mchezo wa
nusu fainali.
Mshambuliaji anayechezea kwa mkopo
akitokea Chelsea Bertrand Traore alifunga goli la kwanza kwa mpira wa
kichwa, kabla ya Kasper Dolberg kufunga la pili baada ya beki
kujichanganya.
Amin Younes alifunga goli la tatu,
lakini Mathieu Valbuena aliipatia matumaini Lyon kwa kuifungia goli
moja hata hivyo baadaye Traore akafunga la nne.
Kasper Dolberg akiifungia Ajax goli la pili
Bertrand Traore akitumbukiza moja ya magoli yake mawili aliyofunga jana
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni