Juventus inakaribia kutinga fainali
ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya pili katika misimu mitatu
wakati Gonzalo Higuain akiifunga mara mbili Monaco katika mchezo wa
kwanza wa nusu fainali.
Wenyeji Monaco wakiwa nyumbani
Ufaransa walianza vyema, huku mchezaji kijana Kylian Mbappe
akimjaribu kipa Gianluigi Buffon kwa mpira wa kichwa na kisha baadaye
akaokoa mchomo mwingine wa chini.
Lakini ilikuwa Higuain aliyetikiza
nyavu akipata msaada wa Dani Alves na kunasa pasi ya kisigino ya
Mbrazili huyo katika dakika ya 29, na kisha baadaye Higuain tena
akaongeza goli la pili katika kipindi cha pili.
Gonzalo Higuain akiachia shuti na kufunga goli la kwanza
Gonzalo Higuain akifunga goli la pili na kuifanya Monaco kutota nyumbani
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni