.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 8 Mei 2017

ARSENAL YATIBUA REKODI YA MANCHESTER UNITED KUTOFUNGWA KATIKA MECHI 25

Arsenal imemaliza rekodi ya Manchester United ya kucheza michezo 25 bila ya kufungwa katika Ligi Kuu ya Uingereza na kuendeleza matumaini ya kumaliza katika nafasi nne za juu.

Baada ya kumaliza kipindi cha kwanza bila kufungana, Granit Xhaka, alifungua goli la kwanza kwa shuti la mbali lililompita juu kipa David de Gea.

Arsenal iliongeza goli la tatu dakika tatu baadaye baada ya Danny Welbeck kuupiga mpira kwa iliyotokana na krosi ya Alex Oxlade-Chamberlain.
                                            Granit Xhaka akiachia shuti na kufunga goli la kwanza
                        Danny Welbeck akiwa ameupiga mpira kwa kichwa na kuzaa goli la pili
Katika mchezo wa kwanza wa awali Liverpool ilitoka sare tasa na Southampton huku James Milner akikosa penati na kusababisha pigo katika mpio za kumaliza nafasi nne za juu.
              Kipa Ben Foster akipangua mpira wa penati iliyopigwa na James Milner

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni