.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 9 Mei 2017

CHELSEA NI KAMA TAYARI MABINGWA WA LIGI KUU YA UINGEREZA

Chelsea ni kama ishakuwa bingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya jana kuilaza Middlesbrough kwa magoli 3-0 ushindi ambao unaifanya Boro kushuka daraja.

Katika mchezo huo uliopigwa katika dimba la Stamford Bridge, Chelsea ilitengeneza nafasi kadhaa na alikuwa Diego Costa aliyefunga kwa pande la Cesc Fabregas.

Chelsea iliandika goli la pili kupitia kwa Marcos Alonso aliyefunga kwa mpira uliopita kati kati ya miguu ya kipa Brad Guzan na Nemanja Matic akafunga goli la tatu.

Kikosi hicho cha kocha Antonio Conte kinaweza kuwa mabingwa Ijumaa iwapo kitapata ushindi katika mchezo wao dhidi ya West Bromwich Albion kwenye dimba la The Hawthorns.
                          Diego Costa akifunga goli la kwanza la Chelsea katika mchezo huo
        Marcos Alonso akifunga goli la pili kwa kupenyeza mpira kati kati ya miguu ya kipa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni