Ndege kubwa ya abiria ya kwanza
kutengenezwa nchini China imefanya safari yake ya kwanza na kuibua
changamoto kwa kampuni kubwa za utengenezaji ndege za Boeing na
Airbus.
Televisheni ya taifa ya nchi hiyo
imeonyesha ndege hiyo iliyotengenezwa na shirika la umma la China
ikiruka bila tatizo lolote ikitokea uwanja wa ndege wa Pudong uliopo
Jijini Shanghai.
Ndege hiyo ni hatua muhimu kwa
China, katika hamasa yake ya kutinga katika soko la dunia kwa uuzaji
ndege.
Shirika hilo la Comac lilipanga
tangu mwaka 2008 kuitengeneza ndege hiyo lakini mpango huo ulikuwa
ukisogezwa mbele kwa muda wote huo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni