Polisi mashariki mwa India katika
jimbo la Bihar wamesema panya wamekunywa maelfu ya lita za pombe
iliyokuwa imekamatwa.
Jimbo la Bihar lilipiga marufuku
uuzaji na unywaji wa pombe mwaka jana na tangu wakati huo polisi
wamekamata lita 900,000 za pombe.
Kamanda wa Polisi wa Mji wa Patna,
Manu Maharaj, amesema ameambiwa wakaguzi wa polisi kuwa kiasi kikubwa
cha pombe iliyokamatwa kimepotea kutokana na panya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni