Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa ESRF, Dkt. Tausi Kida alisema mdahalo huo ni sehemu ya shughuli ambazo zinafanywa na ESRF ili kutazama ni njinsi gani Taasisi inaweza kuisaidia Serikali kuweka mipango thabiti kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Dkt. Kida alisema mdahalo huo ulihusu bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kuangalia utekelezaji wa bajeti zilizopitishwa kwa mwaka wa fedha 2016/2017, changamoto zilizopo na nini kifanyike katika bajeti ya 2017/2018.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni