Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma
ameondoka katika mkutano wa Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi
Duniani (Mei Mosi) baada ya kuzomewa na wafanyakazi wakishinikiza
ajiuzulu urais.
Ngumi pia zimetokea katika mkutano
huo baina ya wafuasi wanaomuunga mkono rais Zuma na wapinzani wake
jambo lililopelekea hotuba zote zilizopangwa kutolewa kwa ajili ya
Mei Mosi kutotolewa.
Shirikisho la Wafanyakazi nchini
humo COSATU, lilitoa wito mwezi uliopita wa kumtaka rais Jacob Zuma
kuachia madaraka baada ya kumfukuza kazi waziri wa fedha
anayekubalika mno.
Licha ya kuwepo kwa shinikizo la
kumtaka kujiuzulu rais Zuma ameapa kubakia madarakani hadi hapo
muhula wake utakapomalizika mwaka 2019.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni