Mwanaume mmoja anayedai kuwa ndiye
mtu mwenye umri mkubwa kuliko wote duniani amefariki dunia akiwa na
umri wa miaka 146, kijijini kwao Java ya Kati nchini Indonesia.
Kwa mujibu wa nyaraka zake,
Sodimedjo, ambaye pia anajulikana kama Mbah Ghoto (Babu Ghoto),
alizaliwa mwezi Desemba mwaka 1870.
Lakini Indonesia kwa wakati huo
ilikuwa haijanza kuweka kumbukumbu za kuzaliwa hadi mwaka 1900, na
kumekuwa na makosa ya uhakika wa umri kabla ya hapo.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni