Juventus imetinga kwa mara ya pili
fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, katika misimu mitatu kwa ushindi
mzuri wa magoli ya jumla 4-1 dhidi ya Monaco.
Ikiwa ilishapata ushindi wa magoli
2-0, timu hiyo ya Italia ilipata goli la kwanza katika mchezo wa jana
kupitia Mario Mandzukic baada ya mpira alioupiga kwa kichwa
kuokolewa.
Dani Alves aliongeza goli la pili
baada ya kuunasa mpira uliopigwa ngumi na kipa Danijel Subasic, huku
Monaco ikipata goli pekee kupitia kwa kinda Kylian Mbappe.
Mario Mandzukic akiifungia Juventus goli la kwanza
Dani Alves akijipinda na kuachia shuti lililoandika goli la pili
Kylian Mbappe akifunga goli kwa shuti la chini lililompita kipa Buffon




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni