.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 7 Mei 2017

LEICESTER CITY YASHINDA NA KUJIHAKIKISHIA KUTOSHUKA DARAJA

Mabingwa watetezi Leicester City imejihakikishia kutokushuka daraja katika Ligi Kuu ya Uingereza, baada ya kupata ushindi wanaostahili wakiwa nyumbani dhidi ya Watford.

Leicester ilipata uongozi kupitia kwa Wilfred Ndidi kuachia shuti umbali wa yadi 10, baada ya Hornets kushindwa kuokoa krosi iliyopigwa na Danny Drinkwater.

Lecester City waligonga mwamba mara mbili kabla ya Riyad Mahrez kuongeza goli la pili kufuatia makosa ya Adrian Mariappa na mpira kumpita Heurelho Gomes.

Marc Albrighton aliongeza goli katika muda wa majeruhi na kufanya matokeo kuwa 3-0, baada ya kunasa pasi ya Jamie Vardy.
                                                     Riyad Mahrez akifunga goli la pili katika mchezo 
                                Marc Albrighton akikamilisha ushindi kwa kufunga goli la tatu 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni