Manchester City wamejiimarisha
katika kuhakikisha wanamaliza katika nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya
Uingereza kwa kupata ushindi mnono wa magoli 5-0 dhidi ya Crystal
Palace na kukwea juu ya Liverpool hadi katika nafasi ya tatu.
Katika mchezo huo David Silva
alifunga goli la kwanza ndani ya dakika mbili tu, likiwa goli
lililofungwa mapema mno katika msimu huu, lakini baada ya hapo
iliwachukua muda mrefu wenyeji Manchester City kuweza kuutawala
mchezo huo.
Kikosi cha Pep Guardiola
kilijihakikishia kuondoka na pointi zote tatu katika kipindi cha pili
baada ya kapteni Vincent Kompany kufunga kupitia krosi ya Kevin de
Bruyne, kisha De Bruyne akifunga la tatu, Raheem Sterling akafunga la
nne na Nicolas Otamendi akahitimisha karamu.
David Silva akiifungia Manchester City goli la kwanza katika mchezo huo
Kapteni Manchester City Vincent Kompany akifunga goli la pili
Raheem Sterling akiachia shuti lililojaa wavunia na kuandika goli la nne




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni