Mchezaji wa Manchester United,
Zlatan Ibrahimovic, ameingia katika orodha ya wanamichezo matajiri
Ulaya akiwa katika nafasi ya pili nyuma ya kinara wa mwaka 2016
Lewis Hamilton.
Ibrahimovic raia wa Sweden
ameingizwa kwenye orodha ya wanamichezo tajiri nchini Uingereza baada
ya kujiunga na Manchester United Julai, mwaka jana.
Akiwa na utajiri wa paundi milioni
110, Ibrahimovic amempiku mchezaji mwenzake wa timu yao Wayne Rooney
anayeshika nafasi ya tatu akiwa na utajiri wa paundi milioni 93.
Dereva wa Formula 1 bingwa wa dunia
Muingereza, Lews Hamilton, anaongoza akiwa na utajiri wa paundi
milioni 131.
Dereva wa mbio za langalanga Lewis Hamilton anaongoza kwa utajiri kwa wachezaji Ulaya


Hakuna maoni :
Chapisha Maoni