.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 2 Mei 2017

RAIS WA ZANZIBAR, DK. SHEIN AONGOZA SHEREHE ZA WAFANYAKAZI KATIKA VIWANJA VYA MAHONDA, UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto, Mhe. Maudline Cyrus Castico alipowasili katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja leo katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar Maalim Khamis Mwinyi alipowasili katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja leo katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia Mkono Wafanyakazi mbali mbali waliopita mbele yake kwa Maandamano wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Baadhi ya wafanyakazi wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba,Sheria,Utumishi wa Umma na Utawala Bora wakipita kwa Maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.
Wafanyakazi na Wananchi kutoka shehia mbali mbali za Unguja walijumuika kwa pamoja katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akiwapungia Mkono Wafanyakazi mbali mbali waliopita mbele yake kwa Maandamano wakati wa Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja akiwa na Viongozi mbali mbali.
Wafanyakazi na Wananchi kutoka shehia mbali mbali za Unguja walijumuika kwa pamoja katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,wakipita kwa maandamano mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo.
Wafanyakazi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakibeba Bango lenye Nembo la Idara yao wakati wa maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Wafanyakazi wa Benki ya Tanzania BOT wakibeba Bango lenye Nembo la Idara yao wakati wa maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja,ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani).
Wafanyakazi wa ​Idara ya Uhamiaji Zanzibar wakimpungia Mkono ​Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),​alipokuwa akipokea ​​maandamano katika Sherehe za Kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani zilizofanyika leo katika viwanja vya Mpira Mahonda Wilaya ya Kaskazini "B" Unguja.Picha na Ikulu, Zanzibar.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni