Timu ya Real Madrid imefikisha
pointi sawa na Barcelona katika kilele cha Ligi Kuu ya Hispania
maarufu kama La Liga baada ya kuichakaza Granada kwa magoli 4-0 na
kupata ushindi wa kirahisi.
Real iliyoshusha kikosi chenye
mabadiliko ya wachezaji tisa, ilikuwa bila Cristiano Ronaldo na
Gareth Bale, lakini ilipata goli la kuongoza ndani ya dakika tatu na
kufikisha manne katika dakika 35.
Katika mchezo huo James Rodriguez
alifunga goli la kwanza akipokea pasi kutoka kwa Lucas Vazquez,
kisha baadaye akafunga goli la pili kwa mpira wa kichwa kabla ya
Alvaro Morata kufunga mengine mawili.
James Rodriguez akishangilia mara baada ya kufunga goli la kwanza
Alvaro Morata akiachia shuti na kufunga goli la tatu la Real Madrid
Katika mchezo wa awali Lionel Messi
alifunga goli lake la 50na 51 katika msimu huu wakati Barcelona
ikiifunga Villarreal kwa magoli 4-1, huku Neymar na Luis Suarez nao
wakifunga goli moja kila mmoja.
Neymar akiwazidi maarifa mabeki wa Villarreal na kufunga goli la kwanza





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni