Wanamgambo wa kundi la Kiislam la
Boko Haram wamewaachia wanafunzi wa kike 82 kati ya 276 waliotekwa
kaskazini mashariki mwa Nigeria miaka mitatu iliyopita.
Ofisi ya rais imesema wanafunzi hao
wameachiwa katika makubaliano ya kubadilishana na watuhumiwa wa kundi
la Boko Haram baada ya mazungumzo.
Wasichana hao watapokelewa na rais
wa Nigeria Muhammadu Buhari katika Jiji la Abuja siku ya leo, kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa.
Kabla ya kuachiwa kwa wanafunzi hao
wa kike, wanafunzi 192 walikuwa bado hawajapatikana tangu
walipotekwa.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni