Cristiano Ronaldo amefunga magoli
mawili wakati Real Madrid ikipiga hatua nyingine katika mbio za
ubingwa wa Ligi Kuu ya Hispania 'La Liga' kwa kuifunga Sevilla 4-1.
Katika mchezo huo Real walifunga
goli la kwanza kupitia kwa Nacho kwa mpira wa adhabu uliotolewa kwa
utata kabla ya Ronaldo kuongeza goli la pili.
Stevan Jovetic alichomoa goli moja
baada ya mapunziko, lakini Ronaldo akafunga goli safi la tatu na
kufikisha magoli 401 akiwa na Real Madrid na Toni Kroos kafunga la
nne.
Cristiano Ronaldo akifunga goli la pili la Real Madrid katika mchezo huo
Kwa matokeo hayo Real Madrid
inabakia katika nafasi ya pili ikiwa na mchezo mmoja mkononi nyumba
ya Barcelona iliyoifunga Las Palmas magoli 4-1 wakati Neymar akifunga
hat-trick katika mchezo huo.
Mchezaji Mbrazili Neymar akionyesha mchoro wa sura ya mama yake katika kuonyesha mapenzi kwa mama katika siku ya mama hapo jana



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni