Seneta mwanamke wa Australia Bi.
Larissa Waters ameweka historia kwa kuwa mwanasiasa wa kwanza
kumnyonyesha mtoto wake ndani ya bunge la taifa la nchi hiyo.
Bi. Waters kutoka chama cha mrengo
wa kushoto cha Greens alimnyonyesha bungeni mtoto wake wa kike wa
miezi miwili aitwae Alia Joy wakati wa upigaji kura siku ya jana.
Bunge la nchi hiyo liliungana na
Seneti mwaka jana kuruhusu wabunge na wawakilishi wanawake
kunyonyesha lakini kulikuwa hakuna mbunge hata mmoja aliyewahi
kufanya hivyo.

Hakuna maoni :
Chapisha Maoni