.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatano, 17 Mei 2017

TIMU YA MANCHESTER CITY YAREJEA KATIKA NAFASI YA TATU LIGI KUU UINGEREZA

Timu ya Manchester City imepata ushindi mzuri wa magoli 3-1 dhidi ya West Brom na kurejea tena katika nafasi ya tatu ya msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza ikiwa imebakiwa na mchezo mmoja.

Iwapo watapata pointi moja tu katika mchezo wao wa jumapili dhidi ya Watford itajihakikishia kumaliza katika nafasi nne za juu katika msimamo na kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Manchester City ilipata goli lake la kwanza kupitia kwa Gabriel Jesus kufuatia mpira ulioanzia kwa Sergio Aguero aliyempasia Kevin de Bruyne, aliyemlisha Jesus.

Mpira wa Aguero uliookolewa usimfikie Jesus ulimkuta De Bruyne na kufunga goli la pili naye Yaya Toure akafunga goli la tatu na Robson-Kanu akafunga goli pekee la Sunderland.
                                            Gabriel Jesus akiifungia Manchester City goli la kwanza
                                            Yaya Toure akitumbukiza goli la tatu la Manchester City
                     Robson-Kanu akifunga goli pekee la West Brom katika mchezo huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni