Magoli kutoka kwa Victor Wanyama na
Harry Kane yameipatia Tottenham ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya
Manchester United katika mchezo wao wa mwisho kucheza katika dimba la
White Hart Lane.
Tottenham Hostspurs wanampango wa
kuwa na uwanja wao mpya, utakaojengwa katika eneo hilo hilo, watakuwa
tayari kwa msimu ujao wa 2018-19 wakicheza michezo ya nyumbani katika
dimba la Wembley msimu ujao.
Katika mchezo wa jana Wanyama
aliipatia Tottenham goli la kwanza kwa mpira wa kichwa katika kipindi
cha kwanza kisha Kane akaongeza la pili katika kipindi cha pili kabla
ya Wayne Rooney kufunga goli pekee la Manchester United.
Victor Wanyama akiruka juu na kufunga goli kwa mpira wa kichwa
Harry Kane akifunga goli la pili la Tottenham
Mkongwe Wayne Rooney akifunga goli pekee la Manchester United




Hakuna maoni :
Chapisha Maoni