.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 4 Juni 2017

WATU SITA WAUWAWA KATIKA SHAMBULIZI LA KIGAIDI JIJINI LONDON

Watu sita wameuwawa na wengine wapatao 48 kujeruhiwa katika shambulizi la kigaidi Jijini London ambapo washambuliaji watatu wanaume nao wameuwawa kwa kupigwa risasi na polisi.

Gari jeupe liliwagonga watembea kwa miguu katika daraja la London jumamosi na kisha watu watatu wakatoka kwenye gari hilo na kuwachoma visu watu kadhaa katika soko Borough lililopo karibu na daraja hilo.

Polisi nchini Uingereza wamesema wanaume hao watatu walikuwa wamevalia vesti feki za mabomu. Mmoja wa majeruhi ni afisa wa polisi ambaye alichomwa kisu wakati alipokuwa anatoa msaada.
Mmoja wa majeruhi akiwa amebebwa kwenye kitanda chenye magurudumu akiwahishwa katika gari la wagonjwa


Hakuna maoni :

Chapisha Maoni