Balozi wa Jamuhuri ya Cuba Nchini
Tanzania Profesa Lucas Domingo Hernandes Kushoto akisalimiana na
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Nyumbani
kwake Jijijini Dar es salaam kwa ajili ya mazungumzo ya urafiki wa
Nchi zao.
Balozi Lucas Domingo Kushoto
akisisitiza azma ya Cuba kuendelea kuunga mkono Kitaaluma Jitihada za
Serikali ya Tanzania na Zanzibar kwa ujumla katika mustawisha miradi
ya Maendeleo.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
Balozi Seif Ali Iddi Kulia akiishukuru Cuba kupitia Balozi Wake kwa
jitihada inazochukuwa za kusaidia Sekta ya Afya Visiwani Zanzibar.
Balozi Lucas Kushoto akimkabidhi
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif zawadi inayovutia ya
Ramani ya Mji wa Havana itakayomsaidia kwa kumbu kumbu zake za
baadae.
Balozi Lucas Domingo Kulia
akimshindikiza Mgeni wake Balozi Seif mara baada ya kumaliza
mazungumzo yao ya ushirikiano wa uhusiano wa Nchi zao mbili {Zanzibar
na Cuba }. Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Jamuhuri ya Watu wa Cuba inakusudia
kuandaa Mpango maalum utakaoziwezesha Wizara zinazosimamia Sekta ya
Utali kati ya Nchi hiyo na Zanzibar kushirikiana katika kuimarisha
huduma za Utalii na masuala yaUtamaduni ili kustawisha urafiki wa
pande hizo.
Balozi wa Cuba Nchini Tanzania
Profesa Lucas Domingo Hernandes alitoa kauli hiyo wakati wa
Mazungumzo yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
Iddi yaliyofanyika kwenye Makaazi yake Mjini Dar es Salaam.
Profesa Lucas Domingo Hernandes
alisema mpango huo utahusisha kuangalia fursa za kuanzishwa kwa
mikataba ya Ushirikiano itakayolenga kuheshimu na kuendeleza uhusiano
ulioanzishwa na Waasisi wa Mataifa hayo Marehemu Fidel Castro wa Cuba
na Mwalimu Julius K. Nyerere wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
Alisema Zanzibar na Cuba ni Visiwa
vyenye mazingira yanavyofanana hasaTamaduni zake kiasi kwamba
juhudi za pamoja zinastahiki kuchukuliwa ili kuona Uchumi, Maendeleo
pamoja na maisha ya Wananchi wa pande hizo mbili yanaendelea kustawi
kila wakati.
Profesa Lucas alisema zipo Sekta
zilizoleta ufanisi na kuifaidisha Jamii kwa kiwango kikubwa tokea
kuanzishwa kwa ushirikiano wa pande hizo mbili akitolea mfano ile ya
Afya ambayo mafanikio yake yameshuhudiwa na Wananchi walio wengi.
Balozi wa Cuba Nchini Tanzania
alimuhakikishia Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Cuba
itaendelea kuunga Mkono jitihada zinazochukuliwa na Tanzania na
Zanzibar kwa ujumla katika kusaidia Taaluma kwenye sekta tofauti za
Maendeleo.
Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Mpango wa Serikali
ya Cuba kupitia Wizara ya Afya Zanzibar wa kusomesha Madaktari
Wazalendo umeleta faraja na kuimarisha uhusiano wa Nchini Mbili hizo.
Balozi Seif alisema yapo mafanikio
makubwa yaliyopatikana katika Sekta ya Afya tokea kumalizika kwa
mafunzo ya awamu ya kwanza ya kundi kubwa la Madaktari Wazalendo
ambapo huduma za matibabu zimezidi kuimarika katika Hospitali na
vituo mbali mbali vya Afya Visiwani Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
alimueleza Balozi Lukas kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
itaendelea kuimarisha ulinzi wa Wahadhiri wa Chuo cha Madaktari
pamoja na Madaktari wanaotoa huduma za Matibabu na Taaluma Zanzibar
licha ya ishara za vitisho iliyowahi kujitokeza dhidi ya wataalamu na
Madaktari hao.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar
8/7/2017.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni