.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 24 Julai 2017

MAJALIWA AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA SONGWE

1
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanyara wilayani Mbozi ambao walikusanyika barabarani wakitaka asimame na kuzungumza nao . Alikuwa akitoka Vwawa kwenda Uwanja wa Ndege wa Songwe Julai 24, 2017.
2
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kushoto kwake) wakiagana na viongozi wa Mkoa wa Songwe kabla ya kuondoka kwenye makazi ya Mkuu wa Mkoa huo kwenda kwenye uwanja wa ndege wa Songwae baada ya kuhitimisha ziara yake mkoani humo Julai 24, 2017.
6
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea silaha za jadi kutoka kwa Chifu Muleshwelwa Mzunda wa Mbozi ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chief wa Songwe Julai 24, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe . Kushoto kwake ni mkewe Mary na watatu kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa.
 
PMO_5595
Baadhi ya watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017.
PMO_5576
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na watumishi wa umma, viongozi wa dini na wananchi katika kikao cha majumuisho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Sunrise wilayani Mbozi Julai 24, 2017. Kulia ni mkewe Mary, kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa na wapili kulia ni Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Songwe, Erasto Zambi.

                                                                                  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni