.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumamosi, 8 Julai 2017

MAMIA WAJITOKEZA KATIKA MAZISHI YA MWANAMUZIKI MKONGWE SHAABAN DEDE

Mamia ya wadau na mashabiki wa muziki wa dansi nchini jana walijitokeza kwa wingi katika maziko ya mwanamuziki mahiri Shaaban Dede aliyefariki dunia katika hospitali ya Taifa Muhimbili juzi asubuhi. Maziko hayo yalifanyika katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.

Shaaban Dede ni mmoja wa wanamuziki mahiri walioutendea haki muziki wa dansi nchini kwa umahiri wake wa kuimba pamoja na utunzi. Mbali ya kuitumikia Msondo Ngoma Music Band hadi umauti yanamkuta, Dede aliwahi kuimba kwa mafanikio makubwa katika bendi za Ddc Mlimani Park, Bima Lee, Safari Sound na Tanzania All Stars.

Baadhi ya nyimbo alizotunga na kupata umaarufu mkubwa ni pamoja na Fatuma akiwa na Msondo Ngoma, Shangwe ya Harusi akiwa na Bima Lee, Talaka Rejea akiwa na Ddc Mlimani Park pamoja nawimbo wa Nyumba ya Mgumba haina Matanga akiwa na Safari Sound.
          Mwili wa marehemu Shaaban Dede ukiingizwa katika makaburi ya Kisutu
Mmiliki wa Rweyunga Blog, Deogratius Rweyunga kulia akiwa na mdau wa muziki wa dansi Phiry Mmari katika maziko hayo
Kiongozi wa DDC Mliman Park, Abdalah Hemba ( mwenye miwani ) akiwasili katika makaburi ya Kisutu.

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni