.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 21 Julai 2017

MANCHESTER UNITED YAIFUNGA MANCHESTER CITY UGENINI

Timu ya Manchester United imepata ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Manchester City katika mchezo uliochezwa Houston nchini Marekani.

Romelu Lukaku na Marcus Rashford walifunga magali hayo mbele ya mashabiki 67,401 katika dimba la NRG.

Lukaku aliyesajiliwa hivi karibuni alimpita kipa wa City Ederson Moraes na kufunga goli akinasa pasi ya Paul Pogba katika dakika ya 37.

Rashford naye akaongeza goli la pili baadaye akinasa pasi ya Jesse Lingard na kufanya matokeo kuwa magoli mawili huku Manchester City wakishindwa kutikisa nyavu.
                             Mshambuliaji Marcus Rashford akijaribu kumpita Kyle Walker 
                                Kipa David De Gea akizuia mchomo wa mshambuliaji Aguero

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni