Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akimkabidhi nyaraka za chama, Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Bw. Abdul Njaidi. (wapili kushoto), ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi majukumu ya kiuongozi jijini Dar es Salaam Julai 20, 2017.
Wengine pichani walioshuhudia hafla hiyo ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshughulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, (watatu kushoto), Bw. Gerald Chami, (wakwanza kushoto), ambaye ni Mweka Hazina Msaidizi na Bw.Peter Malinzi, (kulia), Mweka Hazina aliyemaliza muda wake.
Mwenyekiti wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), ambaye amemaliza muda wake Bw. Innocent Mungy, (wapili kulia), akishuhudia wakati Katibu Mkuu mpya wa chama hicho Bw. Abdul Njaidi. akisaini nyaraka za makabidhiano.NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM
UONGOZI mpya wa Chama cha Maafisa Mawasiliano wa Serikali, (TAGCO), umekabidhiwa rasmi usukani wa kuongoza taasisi hiyo muhimu katika mawasiloiano ya serikali nchini.
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika jijini Dar es Salaam, Julai 20, 2017 ambapo Mwenyekiti wa TAGCO aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy, alimkabidhi “nyenzo” za kufanyia kazi Katibu Mkuu mpya wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi, ambapo shughuli hiyo ilishuhudiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari MAELEZO anayeshuhulikia Huduma za Habari na Picha, Bw. Rodney Thadeus, Mweka Hazina wa chama hicho aliyemaliza muda wake, Bw. Peter Malinzi, Mweka Hazina Msaidizi Mteule, Bw.Gerald Chami.
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Mwenyekliti aliyemaliza muda wake, Bw. Innocent Mungy alisema, “tunawakabidhi TAGCO, hiki ni chombo muhimu sana kwa mawasiliano ya serikali, hivyo hakikisheni mnakiongoza vyema ili maelengo kusudiwa yafikiwe,”.alisema Bw. Mungy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa TAGCO, Bw. Abdul Njaidi alisema, “Tunashukuru kwa kukabidhiwa usukani wa TAGCO, tunajua hiki chombo ni muhimu sana katika kuhakikisha wananchi wanapatiwa taarifa sahihi za shughuli za Serikali yao inazofanya, tutatekeleza majukumu yetu kwa umakini na uaminifu mkubwa, tunaomba ushirikiano kutoka kwa uongozi uliopita na wanachama wote wa TAGCO na watendaji wote serikalini,”. Alisema Bw. Njaidi wakati akitoa neon la shukrani.
Viongozi wengine wapya wa TAGCO ni Bw. Pascal Shelutete (Mwenyekiti), Bi. Sarah Kibonde Msika (Makamu Mwenyekiti), Bi. Tabu Shaibu (Mweka Hazina), Bi. Gaudensia Simwanza (Katibu Msaidizi), Bw. Owen Mwandubya (Katibu Mwenezi) na Bw. Mpokigwa Mwakasipo (Katibu Mwenezi Msaidizi).
TAGCO nichama kinachowa kutanisha pamoja Maafisa Mawasiliano wa Taasisi mbambali za umma, serikali na Halmashauri zote hapa nchini, lengo likiwa ni kupena ujuzi na uwezo wa kuhakikisha taarifa za serikali zinawafikia wananchi kwa usahihi na kwa wakati.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni