Mshambuliaji Marcus Rashford
ametakata kwa kufunga magoli mawili katika mchezo wa kirafiki dhidi
ya LA Galaxy walioibuka na ushindi wa magoli 5-2.
Katika mchezo huo Rashord alifunga
goli la kwanza lililochangiwa na uzembe wa mabeki kisha akaongeza la
pili kufuatia pasi yenye akili ya Juan Mata.
Marouane Fellaini aliongeza goli la
tatu. Katika kipindi cha pili Manchester United ilifanya mabadiliko
ya wachezaji 11 ikimtambulisha rasmi Romelu Lukaku.
Manchester United iliongeza goli la
nne kupitia kwa Henrikh Mkhitaryan akipatiwa pande na Lukaku, kisha
Anthony Martial akafunga goli tano.
Marcus Rashford akifunga goli la kwanza katika mchezo dhidi ya LA Galaxy
Beki wa La Galaxy Ashley Cole akimkata kwanja Romelu Lukaku
David Beckham akifuatilia mchezo wa timu yake ya zamani ya Manchester United dhidi ya La Galaxy
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni