Mwanamke mmoja raia wa New Zealand
amefariki dunia akiwa kisiwa cha Caribbean cha Sint Maarten kutokana
na nguvu ya mgurumo mkubwa wa injini ya ndege ambao ulimuangusha
chini.
Tukio hilo limetokea katika uwanja
wa kimataifa wa Princess Juliana ambao upo mita chache kutoka
baharini.
Polisi wamesema kuwa mwanamke huyo
mwenye umri wa miaka 57 alikuwa ameshikilia uzio wa uwanja wa ndege
kabla ya kusukumwa chini na nguvu ya injini ya ndege iliyokuwa ikipaa
na kuumia vibaya.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni