.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Alhamisi, 20 Julai 2017

PAUNDI MILIONI 196 ZAELEKEA KUMG'OA NEYMAR BARCELONA

Nyota wa Barcelona Neymar anaelekea kung'oka kwenye klabu hiyo na kutua Paris Saint-Germain kwa kitita cha paundi milioni 196.

Barcelona inaonekana kuchukizwa na mwenendo wa Neymar wa kujirusha klabu usiku akiwa na kina Lewis Hamilton na Justin Bieber.

Klabu hiyo inaona starehe za Neymar zinaweza kukatiza kipajichake kama ilivyokuwa kwa Ronaldinho ambaye starehe zilimponza.

Barcelona ipo tayari kuchukua kitita cha paundi milioni 196 kutoka kwa PSG, kisha kutumia fedha hizo kuwanunua Marco Verratti na Kylian Mbappe.
                     Lewis Hamilton, Neymar pamoja na Justin Bieber wakiponda raha pamoja
          Neymar akipata mlo huku akishushia na mvinyo akiwa na wanawake wawili

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni