.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 23 Julai 2017

PEDRO KUREJESHWA UINGEREZA KWA MATIBABU BAADA YA KUGONGANA NA OSPINA CHINA

Mchezaji wa Chelsea, Pedro atarejea Uingereza na kuachana na ziara ya maandalizi ya msimu mpya baada ubongo wake kutikisika na kuumia usoni katika mchezo wa kirafiki walioibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Arsenal huko Beijing.

Pedro mwenye miaka 29, alilazimika kupelekwa hospitali baada ya kugongana na golikipa wa Arsenal David Ospina katika mchezo huo uliochezwa jana.

Taarifa ya klabu ya Chelsea imesema mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania alikuwa chini ya uangalizi usiku mzima wa jana.
   Kipa wa Arsenal David Ospina akigongana na Pedro wakati akiruka kupangua mpira
Pedro akiwa kwenye maumivu makali huku damu zikimchuruzika puani baada ya kugongana na kipa Ospina

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni