.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 4 Agosti 2017

GHOROFA REFU DUNIANI LA MAKAZI YA WATU LAUNGUA MOTO DUBAI

Ghorofa lenye urefu wa futi 1,100 nchini Dubai limeungua moto upande mmoja leo afajiri katika tukio ambalo hata hivyo wakazi wake wote wametoka salama.

Moto huo ulisambaa kwa kasi katika ghorofa hilo la makazi ya watu lililorefu zaidi kuliko yote duniani na kusababisha mtafaruku kwa wakazi wake huku kukiwa na joto la 45c.

Picha za video zinaonyesha jinsi moto huo ulivyokuwa unapanda juu katika ghorofa hilo lenye ghorofa 86, huku sehemu ya moto ukiangukia gari zilizoegesha chini.
                                 Ghorofa refu la makazi Dubai likiwa linawaka moto leo alfajiri
   Magari yaliyokuwa yameegeshwa chini ya ghorofa hiyo yakiwa yameathiriwa na moto huo
Watu wakiangalia moto uliokuwa ukiunguza ghorofa la makazi Dubai hata hivyo moto huo ulidhibitiwa

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni