Romelu Lukaka amefunga magoli mawili
katika mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza akiwa na
Manchester United huku nao Anthony Martial na Paul Poga wakifunga
goli moja kila mmoja.
Katika mchezo huo uliopigwa katika
dimba la Old Traford Lukaku alifunga goli la kwanza katika dakika 33
kwa shuti kali, nyota huyo raia wa Ubelgiji aliongeza goli la pili
katika kipindi cha pili kwa kichwa kiunganisha mpira uliopigwa na
Henrikh Mkhitaryan.
Mfaransa Anthony Martial alifunga
goli la tatu akiingia dimbani kuchukua nafasi ya Marcus Rashford
kisha karamu hiyo ya magoli ilihitimishwa na shuti zuri la mbali
lililopigwa na Paul Pogba katika dakika ya 90.
Romelu Lukaku akifunga goli lake la kwanza katika mchezo huo
Anthony Martial akifunga goli la tatu la Manchester United
Kiungo mshambuliaji Mfaransa Paul Pogba akifunga goli la nne
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni