.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Agosti 2017

MARCOS ALONSO AIBUKA KUWA SHUJAA CHELSEA IKISHINDA


Marcos Alonso ameibuka kuwa shujaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya Tottenham baada ya kuifungia Chelesea magoli mawili na kuiwezesha kuibuka na ushindi wa magoli 2-1.

Katika mchezo huo uliochezwa kwenye dimba la Wembley wageni Chelsea walikuwa wa kwanza kwa goli lililofungwa kwa shuti la mbali na Marcos Alonso.

Tottenham walipata goli la kusawazisha baada ya Michy Batshuayi aliyetokea benchi kujifunga akijaribu kuokoa kwa kichwa mpira uliopigwa na Christian Eriksen, lakini Alonso akaongeza goli la pili.
Shuti la mbali la kiufundi lililopigwa na Marcos Alonso likijaa wavuni na kuiandikia Chelsea goli la kwanza
Michy Batshuayi akijifunga goli katika harakati za kuokoa mpira uliopigwa na
Christian Eriksen

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni