.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Agosti 2017

NEYMAR AIFANYA PSG KUWA MWIBA KWA TIMU ZA LIGI KUU YA UFARANSA

Neymar amezidi kutikisa vichwa vya habari baada ya kufunga magoli mawili na kusaidia kutoa nafasi za kufunga wakati Paris Saint-Germain ikiichakaza Toulouse magoli 6-2.

Katika mchezo huo Max Gradel alikuwa wa kwanza kuipatia Toulouse goli la kushtukiza dhidi ya Paris Saint-Germain katika dakika ya 18 jana usiku.

Lakini Neymar alisawazisha goli hilo dakika 13 baadaye kisha Adrien Rabiot kuongeza goli la pili akisaidiwa na Neymar huku Edinson Cavani akiongeza goli la tatu kwa mkwaju wa penati.

Toulouse ikapata goli la pili kupitia kwa Thiago Silva aliyejifunga, hata hivyo PSG wakaongeza magoli mengine kupitia kwa Javier Pastore, Layvin Kurzawa na Neymar.
          Mshambuliaji nyota wa PSG Mbrazili Neymar akiachia shuti na kufunga goli
   Mbrazili Neymar akitumbukiza goli lake la pili katika mchezo huo walioibuka na ushindi mnono

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni