.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumatatu, 21 Agosti 2017

TIMU ZA BARCELONA NA REAL MADRID ZAANZA KWA USHINDI LA LIGA

Timu ya Barcelona imeibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya Real Betis ushindi uliochangiwa na jitihada za nyota wao Lionel Messi katika mechi yao ya kwanza ya La Liga.

Katika mchezo huo Barcelona walikuwa wamevalia jezi ambazo zina jina la mji wao mgongoni katika kuomboleza watu waliouwawa katika tukio la ugaidi.

Barcelona walipata goli lao la kwanza kupitia kwa Alin Tosca aliyejifunga akijaribu kuzuia krosi ya Gerard Deulofeu na kisha Sergi Roberto kufunga goli la pili kwa penati.
      Alin Tosca akiangalia mpira aliougonga kimakosa ukimshinda kipa wao na kutinga wavuni
                          Mchezaji Sergi Roberto akifunga goli la pili kwa mkwaju wa penati
Wakati huo huo mabingwa watetezi Real Madrid nao wameanza La Liga kwa ushindi wa magoli 3- dhidi ya Deportivo, huku Gareth Bale, Casemiro na Toni Kroos wakifunga magoli hayo.
Sergio Ramos akipewa kadi nyekundu na kutolewa uwanjani baada ya kupata kadi mbili za njano katika mchezo huo

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni