.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 18 Agosti 2017

MTUKUTU DIEGO COSTA AZIDI KUIWEKEA NGUMU CHELSEA

Vita ya Diego Costa na Chelsea imepamba moto baada ya mshambuliaji huyo kukataa ombi la kurejea London na kusisitiza hana mpango wa kuondoka nchini Brazili na kwa sasa anajifua kwenye gym.

Costa kwa sasa anaishi nyumbani kwao katika mji wa Lagarto baada ya meneja Antonio Conte kumtumia ujumbe wa maandishi uliomueleza hayupo tena katika mipango yake ya Chelsea.

Costa pia amedai kuwa Chelsea inataka kumlazimisha kufanya mazoezi na kikosi cha akiba iwapo atarejea. Tayari amepigwa faini ya laki 3 na huenda akapigwa faini nyingine akiendelea kugoma kurejea.
              Diego Costa akiwa kwenye gym nchini Brazili baada ya kugoma kurejea Chelsea

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni