Wanandoa wazee waliofunga ndoa
iliyodumu kwa miaka 65 wamekufa wakiwa wameshikana mikono kufuatia
ombi lao la kuuwawa kwa kutumia dawa inayosababisha kifo kisicho na
machungu kutekelezwa.
Wanandoa hao Nic na Trees
Elderhorst, wote wenye umri wa miaka 91, waliaga dunia wakiwa
wamezungukwa na wanafamilia nyumbani kwao huko Didam, nchini
Uholanzi.
Wanandoa hao waliwasilisha ombi la
kufa pamoja kutokana na Nic kuwa mgonjwa na Trees kukosa uwezo wa
kumuhudumia mumewe mgonjwa kutokana naye kuwa mgonjwa.
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni