Cristiano Ronaldo amefunga goli na
kisha akatolewa nje kwa kadi nyekundu wakati Real Madrid ikiifunga
Barcelona magoli 3-1 katika mchezo wa kwanza wa kombe la Super Cup.
Katika mchezo huo Gerard Pique
alijikuta akijifunga kwa kutumbukiza mpira katika goli lao akijaribu
kukoa krosi ya Marcelo kabla ya Lionel Messi kusawazisha kwa mkwaju
wa penati.
Ronaldo, aliyetokea benchi alifunga
goli la pili la Real Madrid baada ya kutoka mbio na mpira umbali wa
nusu ya kiwanja.
Ronaldo alipewa kadi ya kwanza kwa
kushangilia goli hilo kwa kuvua jezi na kisha baadaye akapewa kadi ya
pili kwa kujiangusha, kabla ya Marco Asensio kufuga goli la tatu.
Gerard Pique akijifunga goli wakati akijaribu kuokoa mpira
Cristiano Ronaldo akishika kichwa asiamini baada ya refa kumpa kadi ya pili ya njano
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni