Neymar amefunga goli la kwanza akiwa
na Paris St-Germain katika mchezo wake wa kwanza tangu asajiliwe kwa
dau lililoweka rekodi la paundi milioni 200 kutoka Barcelona.
Mchezaji huyo raia wa Brazili
alikuwa na mchango katika magoli yote matatu ya PSG na kuifanya timu
yake kuendelea kufanya vyema kwa asilimia 100.
Jordan Ikoko alifunga goli la kwanza
baada ya kujifunga kimakosa wakati akizuia pande la Neymar lisimfikie
Cavani.
Neymar tena akigongeana vyema mpira
na Cavani na kisha naye kutoa pande zuri kwa Neymar ambaye alifunga
katika umbali wa yadi sita.
Mbrazil Neymar akiachia shuti na kufunga goli lake la kwanza akiwa na PSG
Wachezaji wa PSG wakimpongeza Neymar baada ya kufunga goli la tatu
Hakuna maoni :
Chapisha Maoni