.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumanne, 1 Agosti 2017

ZIARA YA MAJALIWA CHUNYA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mwenyekiti wa Makampuni ya SUNSHINE GROUP, Betty Mkwasa wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa Sunshine Mining Limited uliopo Chunya Agosti 1, 2017, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka Dennis Dillip ambaye ni Mjiolojia kuhusu mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni ya Sunshine Mining Limited uliopo Chunya wakati alipoutembelea Agosti 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Amos Makalla wakipata Maelezo kutoka kwa Afisa Madini wa Mkoa wa Mbeya Mhandisi Said Mkwawa kuhusu taarifa za Kampuni ya Sunshine Gold Mininga Limited wakati alipotembelea mtambo wa kusafisha dhahabu wa kampuni hiyo wilayani Chunya Agosti 1, 2017. (Picha na Pfisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifurahia wimbo maalum unaozungumzia utendaji wa serikali ya Awamu ya Tano ulioimbwa na Kwaya maarufu ya Kiwete katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu kwenye uwanja wa Sabsaba mjini Chunya Julai 1, 2017, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Sabasaba  mjiini Chunya Agosti 1, 2017.  Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Mbeya. (PIcha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea mkuki  kutoka kwa Mbunge wa Lupa, Victor Mwambalaso ikiwa ni ishara ya kusimikwa kuwa Chifu wa makabila ya Wakimbu na Wasafa katika mkutano wa hadhara aliouhutubia  kwenye uwanja wa Sabasaba mjini Chunya Agosti 1, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni