.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Ijumaa, 22 Septemba 2017

DIEGO COSTA AKWEA PIPA KUELEKEA HISPANIA

Mchezaji anayeondoka Chelsea Diego Costa amekwea pipa akitokea Brazil kwenda Hispania akitarajia kujiunga tena na klabu yake ya Atletico Madrid kwa dau nono.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania amesema hana kinyongo na kocha Antonio Conte, licha ya kocha huyo kumtumia arafa isemayo hana mpango naye.

Hatimaye Costa amekubali kurejea kwenye klabu yake hiyo ya zamani ya Atletico, ambapo uhamisho wake utakamilishwa Januari, baada ya kuondolewa katazo la kusajili La Liga.
Diego Costa akiagana na watu katika uwanja wa ndege wa Brazil kabla ya kupanda ndege kuelekea Hispania

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni