.

.

.

.

.

.

.

.
KARIBUNI TUHABARIKE, TUELIMISHANE, TUPEANE HABARI ZA KUKUFANYA UTABASAMU KIDOGO NA MATUKIO YALIYOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA TOKA KILA PEMBE CONTACTS: +255 787 377 722 Email: drweyunga@gmail.com PIA UNAWEZA KUNI FOLLOW KUPITIA INSTAGRAM YANGU @drweyunga | TANGAZA NASI ILI UWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI.

Jumapili, 22 Oktoba 2017

ARSENAL YAIZAMISHA EVERTON, ROONEY AKITUPIA KAMA LA 2002

Kocha Ronald Koeman amesema ataibadilisha Everton na kuweza kufanya vizuri baada ya kuporomoka mkiani kufuatia kipigo cha magoli 5-2 dhidi ya Arsenal katika dimba la Goodison Park.

Everton walijikuta wakiaibika kwa kipigo hicho mbele ya mashabiki wao, ambapo hadi sasa hawajapata ushindi katika michezo mitano katika michuano yote.Wayne Rooney alifunga goli la kwanza kama alilowafunga Arsenal mwaka 2002.

Nacho Monreal aliisawazishia Arsenal goli, kabla ya baadaye Mesut Ozil akaongeza goli la pili Alexandre Lacazette akatumbukiza la tatu na Aaron Ramsey, Oumar Niasse akaifungia Everton kabla ya Alexis Sanchez kufunga goli la tano.
   Wayne Rooney akipiga mpira wa shuti la kuzungusha na kukumbushia alivyoitungua Arsenal mwaka 2002
     Oumar Niasse akiifungia Everton goli la pili katika mchezo huo ulioishia kwa kufungwa magoli 5-2 na Arsenal 

Hakuna maoni :

Chapisha Maoni