Bondia Anthony Joshua ametetea
mikanda yake ya uzito wa juu ya WBA na IBF baada ya kuibuka na
ushindi kufuatia refa kusitisha kiutata pambano hilo katika raundi ya
10 dhidi ya Carlos Takam.
Katika pambano hilo Muingereza
Joshua, 28, aliumia pua yake baada ya kugongana kwa nguvu kwa kichwa
na Takam mapema katika pambano hilo na bondia huyo ambaye
aliyejiandaa kwa pambano hilo kwa siku 12.
Takam ilibidi achunguzwe mara mbili
na madaktari kutokana na kipigo kabla ya kuzidiwa zaidi katika raundi
ya 10 pale refa Phil Edwards alipoingilia kati kusimamisha pambano
hilo hatua ambayo haikuwafurahisha mashabiki na kuzomea.
Bondia Anthony Joshua akimshindilia ngumi ya kulia bondia Carlos Takam
Anthony Joshua akimshindilia ngumi nzito Carlos Takam katika pambano hilo
Bondia Carlos Takam akianguka chini baada ya kushindiliwa ngumi na Anthony Joshua
Refa Phil Edwards akiingilia kati na kusimamisha pambano baada ya Takam kuzidiwa





Hakuna maoni :
Chapisha Maoni