Kocha Arsene Wenger ameanza kuchonga
kwa kusema kuwa kikosi chake cha Arsenal kimewaumbua wakosoaji baada
ya kutokea nyuma kufungwa na kuibuka na ushindi katika michezo mitatu
mfululizo.
Aaron Ramsey aliifungia Arsenal goli
la ushindi dhidi ya Swansea, katika mchezo wa Ligi Kuu ya Uingereza
ambao Sam Clucas aliifungia Swansea goli la kwanza lakini Sead
Kolasinac akaisawazishia Arsenal.
Katika kuonyesha upambanaji Arsenal
ilifungwa kwanza goli na Rverton na Swansea katika michezo ya ligi,
na pia kufungwa kwanza na Norwich katika kombe la Carabao lakini
wakaibuka na ushindi.
Sead Kolasinac akiachia shuti kali lililojaa wavuni na kuiandikia Arsenal goli la kusawazisha
Aaron Ramsey akiifungia Arsenal goli la ushindi katika mchezo huo kwenye dimba la Emirates



Hakuna maoni :
Chapisha Maoni